Chicago
London
Dar Es Salaam
 
 

Diamond Kuja Na Video Ya Mdogo Mdogo Remix

News by : Staff Reporter
 
23 Jul, 2014 23:55:42
 
//
 

BAADA ya kufanya vizuri na video ya ngoma yake ya ‘Mdogo mdogo’, nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, ameamua kutengeneza nyingine.

 

Video hiyo iliyosambazwa mapema mwezi huu, inaendelea kujizolea umaarufu kutokana na ubora wake.

 

Kupitia ukurasa wake wa instagram, msanii huyo ameandika kuwa kama kuna mtu anahisi ana staili bomba inayoweza kuendana na wimbo huo, awasiliane naye kupitia ukurasa huo na atampatia zawadi ya shilingi milioni moja.

 

“Nimeona ‘Mdogo mdogo’ imefanya vizuri, hivyo nataka kuifanyia remix kwa kutoa video nyingine ambayo nataka nitulie kuiandaa ili kuleta changamoto katika soko langu,” alisema.

 

Mbali ya ‘Mdogo mdogo,’ Diamond anatamba na kazi nyingine matata ya ‘Bum bum’ aliyomshirikisha Mnigeria, Iyanya.

 

Diamond Platnumz - Mdogo Mdogo

 

 

 
 
 
 
 
Copyright © 2011 Bongo Radio. Subsidiary of Bongo Media Group. All Rights Reserved
Valid XHTML 1.0 Transitional