Chicago
London
Dar Es Salaam
 
 

Alikiba Atoa Nyimbo Mbili Mpya Kwa Mpigo Ni Mwana na Kimasomaso

News by : Staff Reporter
 
24 Jul, 2014 21:33:57
 
//
 
Baada ya kimya kirefu nyota wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania Ally Kiba au kama anavyojulikana na wapenzi wake wengi kwa jina la la kimuziki la Alikiba amtoa nyimbo mbili kali kwa mpigo.

Inaweza kuonekana Alikiba anafuata nyayo za Diamond ambaye nae siku chache zilizopita alitoa video mbili kwa mpigo, tofauti na Diamond, Alikiba ni msanii ambaye hajasikika masikioni mwa wapenzi wa Bongo Flava kwa muda mrefu sana kwa hiyo utoaji wake wa nyimbo hizi mbili umekuwa ukisubiriwa kwa hamu sana na wapenzi wengi wa muziki wa Bongo Flava.

Nyimbo zote mbili alizozitoa ya Mwana na Kimasomaso zina mahadhi na mirindimo ya Pwani. Kimasomaso ambayo ni nyimbo maarufu sana kwa wapenzi wengi wa muziki Tanzania na Afrika Mashariki ameifanyia marudio kutoka kwa hayati Issa Matona.imbop

Isikilize nyimbo ya Alikiba ya Mwana kutoka tovuti maarufu ya muziki na burudani ya EastAfricanTube kwa kubonyeza hapo chini.

Alikiba - Mwana
 
 
 
 
 
Copyright © 2011 Bongo Radio. Subsidiary of Bongo Media Group. All Rights Reserved
Valid XHTML 1.0 Transitional