Chicago
London
Dar Es Salaam
 
 

Vanessa Mdee Azungumzia Fitna Katika Muziki Tanzania

News by : Staff Reporter
 
07 Nov, 2014 00:36:36
 
//
 

Dar es Salaam - Mwanamuziki wa kike, Vanessa Mdee maarufu kwa jina la Vee Money, amewataka wasanii kujituma katika kazi na kuachana na fikra hasi anazoamini ni kikwazo kwa walio wengi.

 

Vee Money, aliyeonekana kwenye shoo ya Kourtney And Khloe Take The Hamptons (The Kardashians) inayoonyeshwa na kituo cha E! Entertainment cha Marekani, wikiendi iliyopita aliliambia gazeti hili kuwa wengi huathirika kisaikolojia kutokana na mawazo hasi wanayokuwa nayo hasa wanapokutana na changamoto ambazo ni za kawaida katika utafutaji.

 

“Walio wengi hupata fikra hasi hasa wanapokumbana na changamoto. Ijulikane kwamba hakuna anayefanya kazi bila kupata vikwazo, hakuna kazi nyepesi. Sasa wakikumbana nazo wanaamini kwamba kuna fitina za mtu au watu,” alisema msanii huyo anayetamba na wimbo wake wa “Hamjui”. Akielezea mtazamo wake katika hilo, Vee Money alisema haamini kama kuna fitina katika muziki na katu hawezi kupoteza muda kufikiria mambo kama hayo.

 

“Sina imani hizo na hata kama ikija kunitokea sitaamini bali nitajua ni sehemu ya changamoto za kikazi au maisha kisha nitasonga mbele. Unajua tunapoteza muda kwa kuwa na imani potofu, hata kama fitna zitakuwepo onyesha uwezo wako usikubali zikupoteze,” alisema.

 

Alisema wasanii wengi hupotea kutokana na kuamini nguvu ya fitna na mwisho wa siku wanashuka kimuziki. “Wengi wanashuka kimuziki kwa kukosa plan B, japokuwa wengine hulewa sifa na kutokuwa na usimamizi mzuri ni moja ya sababu pia,” alisema Vee Money.

SOURCE: Mwananchi

Last News
 
 
 
 
 
Copyright © 2011 Bongo Radio. Subsidiary of Bongo Media Group. All Rights Reserved
Valid XHTML 1.0 Transitional